Native Bible

Acts 15:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Simoni amekwisha kutueleza jinsi Mungu, kwa mara ya kwanza alivyoonyesha kuhusika kwa kujichagulia watu kutoka watu wa Mataifa kwa ajili ya Jina lake.

Acts 15:14 in English

Acts 15:14 · Berean Standard Bible

Simon * has told us how God first visited the Gentiles to take from them a people to be His own.

Context

12Kusanyiko lote likakaa kimya, wakawasikiliza Paulo na Barnaba wakieleza jinsi Mungu alivyowatumia kutenda ishara na maajabu kwa watu wa Mataifa. 13Walipomaliza kunena, Yakobo akasema, “Ndugu zangu, nisikilizeni. 14Simoni amekwisha kutueleza jinsi Mungu, kwa mara ya kwanza alivyoonyesha kuhusika kwa kujichagulia watu kutoka watu wa Mataifa kwa ajili ya Jina lake. 15Maneno ya manabii yanakubaliana na jambo hili, kama ilivyoandikwa: 16“ ‘Baada ya mambo haya nitarudi, nami nitajenga upya nyumba ya Daudi iliyoanguka. Nitajenga tena magofu yake na kuisimamisha,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.