Matendo 10:16
Acts 10:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Jambo hili lilitokea mara tatu na ghafula ile nguo ikarudishwa mbinguni.
Acts 10:16 in English
Acts 10:16 · Berean Standard Bible
This happened three times, and all at once the sheet was taken back up into heaven.
Context
14Petro akajibu, “La hasha Bwana! Sijawahi kamwe kula kitu chochote kilicho najisi.” 15Ile sauti ikasema naye mara ya pili, “Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa.” 16Jambo hili lilitokea mara tatu na ghafula ile nguo ikarudishwa mbinguni. 17Wakati Petro akiwa bado anajiuliza kuhusu maana ya maono haya, wale watu waliokuwa wametumwa na Kornelio wakaipata nyumba ya Simoni mtengenezaji wa ngozi wakawa wamesimama mbele ya lango. 18Wakabisha hodi na kuuliza kama Simoni aliyeitwa Petro alikuwa anaishi hapo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.