Native Bible

2 Kings 6:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha mmoja wao akasema, “Je, tafadhali, huwezi kufuatana na watumishi wako?” Elisha akajibu, “Nitakuja.”

2 Kings 6:3 in English

2 Kings 6:3 · Berean Standard Bible

Then one of them said, “Please come with your servants.” “I will come,” he replied.

Context

1Wana wa manabii wakamwambia Elisha, “Tazama, mahali hapa tunapokutana nawe ni padogo sana kwetu. 2Twendeni Yordani, mahali ambapo kila mmoja wetu anaweza kupata nguzo moja, nasi tujenge huko mahali petu pa kuishi.” Naye akawaambia, “Nendeni.” 3Kisha mmoja wao akasema, “Je, tafadhali, huwezi kufuatana na watumishi wako?” Elisha akajibu, “Nitakuja.” 4Naye akaenda pamoja nao. Basi wakaenda Yordani, nao wakaanza kukata miti. 5Mmoja wao alipokuwa anakata mti, shoka lilitumbukia kwenye maji. Akalia, “Ee bwana wangu, shoka lilikuwa la kuazima!”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.