2 Wafalme 6:5
2 Kings 6:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mmoja wao alipokuwa anakata mti, shoka lilitumbukia kwenye maji. Akalia, “Ee bwana wangu, shoka lilikuwa la kuazima!”
2 Kings 6:5 in English
2 Kings 6:5 · Berean Standard Bible
As one of them was cutting down a tree, the iron axe head fell into the water. “Oh, my master,” he cried out, “it was borrowed!”
Context
3Kisha mmoja wao akasema, “Je, tafadhali, huwezi kufuatana na watumishi wako?”
Elisha akajibu, “Nitakuja.” 4Naye akaenda pamoja nao.
Basi wakaenda Yordani, nao wakaanza kukata miti. 5Mmoja wao alipokuwa anakata mti, shoka lilitumbukia kwenye maji. Akalia, “Ee bwana wangu, shoka lilikuwa la kuazima!” 6Mtu wa Mungu akauliza, “Je, liliangukia wapi?” Alipomwonyesha mahali penyewe, Elisha akakata kijiti na kukitupa mahali pale, nalo shoka likaelea. 7Akasema, “Lichukue.” Kisha yule mtu akanyoosha mkono wake, akalichukua.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.