2 Wafalme 6:4
2 Kings 6:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naye akaenda pamoja nao. Basi wakaenda Yordani, nao wakaanza kukata miti.
2 Kings 6:4 in English
2 Kings 6:4 · Berean Standard Bible
So Elisha went with them, and when they came to the Jordan, they began to cut down some trees.
Context
2Twendeni Yordani, mahali ambapo kila mmoja wetu anaweza kupata nguzo moja, nasi tujenge huko mahali petu pa kuishi.”
Naye akawaambia, “Nendeni.” 3Kisha mmoja wao akasema, “Je, tafadhali, huwezi kufuatana na watumishi wako?”
Elisha akajibu, “Nitakuja.” 4Naye akaenda pamoja nao.
Basi wakaenda Yordani, nao wakaanza kukata miti. 5Mmoja wao alipokuwa anakata mti, shoka lilitumbukia kwenye maji. Akalia, “Ee bwana wangu, shoka lilikuwa la kuazima!” 6Mtu wa Mungu akauliza, “Je, liliangukia wapi?” Alipomwonyesha mahali penyewe, Elisha akakata kijiti na kukitupa mahali pale, nalo shoka likaelea.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.