2 Wakorintho 3:16
2 Corinthians 3:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini wakati wowote mtu anapomgeukia Bwana, utaji unaondolewa.
2 Corinthians 3:16 in English
2 Corinthians 3:16 · Berean Standard Bible
But whenever anyone turns to the Lord, the veil is taken away.
Context
14Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana mpaka leo utaji ule ule hufunika wakati Agano la Kale linasomwa. Huo utaji haujaondolewa, kwa maana ni katika Kristo peke yake unaondolewa. 15Hata leo Sheria ya Mose inaposomwa, utaji hufunika mioyo yao. 16Lakini wakati wowote mtu anapomgeukia Bwana, utaji unaondolewa. 17Basi Bwana ndiye Roho. Mahali alipo Roho wa Bwana hapo pana uhuru. 18Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji tunadhihirisha utukufu wa Bwana, kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, utokao kwa Bwana, ambaye ndiye Roho.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.