2 Wakorintho 3:14
2 Corinthians 3:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana mpaka leo utaji ule ule hufunika wakati Agano la Kale linasomwa. Huo utaji haujaondolewa, kwa maana ni katika Kristo peke yake unaondolewa.
2 Corinthians 3:14 in English
2 Corinthians 3:14 · Berean Standard Bible
But their minds were closed. For to this day the same veil remains at the reading of the old covenant. It has not been lifted, because only in Christ can it be removed.
Context
12Kwa hiyo, kwa kuwa tunalo tumaini hili, tuna ujasiri sana. 13Sisi si kama Mose, ambaye ilimpasa kuweka utaji ili kufunika uso wake ili Waisraeli wasiuone ule mngʼao uliokuwa juu yake hadi ulipofifia na hatimaye kutoweka. 14Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana mpaka leo utaji ule ule hufunika wakati Agano la Kale linasomwa. Huo utaji haujaondolewa, kwa maana ni katika Kristo peke yake unaondolewa. 15Hata leo Sheria ya Mose inaposomwa, utaji hufunika mioyo yao. 16Lakini wakati wowote mtu anapomgeukia Bwana, utaji unaondolewa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.