2 Wakorintho 3:13
2 Corinthians 3:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sisi si kama Mose, ambaye ilimpasa kuweka utaji ili kufunika uso wake ili Waisraeli wasiuone ule mngʼao uliokuwa juu yake hadi ulipofifia na hatimaye kutoweka.
2 Corinthians 3:13 in English
2 Corinthians 3:13 · Berean Standard Bible
We are not like Moses, who would put a veil over his face to keep the Israelites from gazing at the end of what was fading away.
Context
11Ikiwa kile kilichokuwa kinafifia kilikuja kwa utukufu, je, si zaidi utukufu wa kile kinachodumu? 12Kwa hiyo, kwa kuwa tunalo tumaini hili, tuna ujasiri sana. 13Sisi si kama Mose, ambaye ilimpasa kuweka utaji ili kufunika uso wake ili Waisraeli wasiuone ule mngʼao uliokuwa juu yake hadi ulipofifia na hatimaye kutoweka. 14Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana mpaka leo utaji ule ule hufunika wakati Agano la Kale linasomwa. Huo utaji haujaondolewa, kwa maana ni katika Kristo peke yake unaondolewa. 15Hata leo Sheria ya Mose inaposomwa, utaji hufunika mioyo yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.