2 Wakorintho 3:12
2 Corinthians 3:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo, kwa kuwa tunalo tumaini hili, tuna ujasiri sana.
2 Corinthians 3:12 in English
2 Corinthians 3:12 · Berean Standard Bible
Therefore, since we have such a hope, we are very bold.
Context
10Kwa maana kile kilichokuwa na utukufu sasa hakina utukufu ukilinganisha na huu utukufu unaozidi wa Agano Jipya. 11Ikiwa kile kilichokuwa kinafifia kilikuja kwa utukufu, je, si zaidi utukufu wa kile kinachodumu? 12Kwa hiyo, kwa kuwa tunalo tumaini hili, tuna ujasiri sana. 13Sisi si kama Mose, ambaye ilimpasa kuweka utaji ili kufunika uso wake ili Waisraeli wasiuone ule mngʼao uliokuwa juu yake hadi ulipofifia na hatimaye kutoweka. 14Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana mpaka leo utaji ule ule hufunika wakati Agano la Kale linasomwa. Huo utaji haujaondolewa, kwa maana ni katika Kristo peke yake unaondolewa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.