2 Nyakati 17:14
2 Chronicles 17:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakaandikishwa katika jamaa zao kama ifuatavyo: Kutoka Yuda, majemadari wa vikosi vya elfu: Jemadari Adna akiwa na askari wa vita 300,000;
2 Chronicles 17:14 in English
2 Chronicles 17:14 · Berean Standard Bible
These are their numbers according to the houses of their fathers: From Judah, the commanders of thousands: Adnah the commander, and with him 300,000 mighty men of valor;
Context
12Yehoshafati akaendelea kupata nguvu zaidi na zaidi, akajenga ngome na miji ya hazina katika Yuda 13na akawa na wingi mkubwa wa vitu katika miji ya Yuda. Pia aliweka askari wa vita wenye uzoefu huko Yerusalemu. 14Wakaandikishwa katika jamaa zao kama ifuatavyo:
Kutoka Yuda, majemadari wa vikosi vya elfu:
Jemadari Adna akiwa na askari wa vita 300,000; 15aliyefuata ni jemadari Yehohanani, akiwa na askari 280,000 walio tayari kwa vita; 16aliyefuata ni Amasia mwana wa Zikri, ambaye alijitolea kwa ajili ya kazi ya Bwana, akiwa na askari 200,000.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.