1 Wathesalonike 5:4
1 Thessalonians 5:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bali ninyi, ndugu, hampo gizani hata siku ile iwakute ghafula kama mwizi.
1 Thessalonians 5:4 in English
1 Thessalonians 5:4 · Berean Standard Bible
But you, brothers, are not in the darkness so that this day should overtake you like a thief.
Context
2kwa kuwa mnajua vyema kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajapo usiku. 3Wakati watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwanamke mwenye mimba; nao hakika hawatatoroka. 4Bali ninyi, ndugu, hampo gizani hata siku ile iwakute ghafula kama mwizi. 5Ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi si wana wa giza wala wa usiku. 6Kwa hiyo basi, tusilale kama watu wengine walalavyo, bali tukeshe na kuwa na kiasi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.