1 Wathesalonike 5:3
1 Thessalonians 5:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwanamke mwenye mimba; nao hakika hawatatoroka.
1 Thessalonians 5:3 in English
1 Thessalonians 5:3 · Berean Standard Bible
While people are saying, “Peace and security,” destruction will come upon them suddenly, like labor pains on a pregnant woman, and they will not escape.
Context
1Basi, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira hatuna haja ya kuwaandikia, 2kwa kuwa mnajua vyema kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajapo usiku. 3Wakati watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwanamke mwenye mimba; nao hakika hawatatoroka. 4Bali ninyi, ndugu, hampo gizani hata siku ile iwakute ghafula kama mwizi. 5Ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi si wana wa giza wala wa usiku.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.