Native Bible

1 Samuel 3:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha Bwana akamwita Samweli. Samweli akajibu, “Mimi hapa.”

1 Samuel 3:4 in English

1 Samuel 3:4 · Berean Standard Bible

Then the LORD called to Samuel, and he answered, “Here I am.”

Context

2Usiku mmoja Eli, ambaye macho yake yalikuwa yamefifia sana kiasi kwamba aliona kwa shida sana, alikuwa amelala mahali pake pa kawaida. 3Taa ya Mungu bado ilikuwa haijazimika, na Samweli alikuwa amelala Hekaluni* mwa Bwana, ambapo Sanduku la Mungu lilikuwako. 4Kisha Bwana akamwita Samweli. Samweli akajibu, “Mimi hapa.” 5Naye akakimbia kwa Eli na kumwambia, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.” Lakini Eli akasema, “Sikukuita; rudi ukalale.” Hivyo akaenda kulala. 6Bwana akaita tena, “Samweli!” Naye Samweli akaamka, kwenda kwa Eli na kusema, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.” Eli akasema, “Mwanangu, sikukuita, rudi ukalale.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.