Native Bible

1 Samuel 3:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Taa ya Mungu bado ilikuwa haijazimika, na Samweli alikuwa amelala Hekaluni* mwa Bwana, ambapo Sanduku la Mungu lilikuwako.

1 Samuel 3:3 in English

1 Samuel 3:3 · Berean Standard Bible

Before the lamp of God had gone out, Samuel was lying down in the temple of the LORD, where the ark of God was located.

Context

1Kijana Samweli alihudumu mbele za Bwana chini ya Eli. Katika siku zile neno la Mungu lilikuwa adimu, hapakuwepo na maono mengi. 2Usiku mmoja Eli, ambaye macho yake yalikuwa yamefifia sana kiasi kwamba aliona kwa shida sana, alikuwa amelala mahali pake pa kawaida. 3Taa ya Mungu bado ilikuwa haijazimika, na Samweli alikuwa amelala Hekaluni* mwa Bwana, ambapo Sanduku la Mungu lilikuwako. 4Kisha Bwana akamwita Samweli. Samweli akajibu, “Mimi hapa.” 5Naye akakimbia kwa Eli na kumwambia, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.” Lakini Eli akasema, “Sikukuita; rudi ukalale.” Hivyo akaenda kulala.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.