Native Bible

1 Samuel 3:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kijana Samweli alihudumu mbele za Bwana chini ya Eli. Katika siku zile neno la Mungu lilikuwa adimu, hapakuwepo na maono mengi.

1 Samuel 3:1 in English

1 Samuel 3:1 · Berean Standard Bible

And the boy Samuel ministered to the LORD before Eli. Now in those days the word of the LORD was rare and visions were scarce.

Context

1Kijana Samweli alihudumu mbele za Bwana chini ya Eli. Katika siku zile neno la Mungu lilikuwa adimu, hapakuwepo na maono mengi. 2Usiku mmoja Eli, ambaye macho yake yalikuwa yamefifia sana kiasi kwamba aliona kwa shida sana, alikuwa amelala mahali pake pa kawaida. 3Taa ya Mungu bado ilikuwa haijazimika, na Samweli alikuwa amelala Hekaluni* mwa Bwana, ambapo Sanduku la Mungu lilikuwako.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.