1 Samweli 18:3
1 Samuel 18:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yonathani akafanya agano na Daudi kwa sababu alimpenda kama nafsi yake mwenyewe.
1 Samuel 18:3 in English
1 Samuel 18:3 · Berean Standard Bible
Then Jonathan made a covenant with David because he loved him as himself.
Context
1Baada ya Daudi kumaliza kuongea na Sauli, roho ya Yonathani ikaambatana na roho ya Daudi, naye akampenda kama nafsi yake mwenyewe. 2Kuanzia siku ile Sauli akamchukua Daudi naye hakumruhusu kurudi nyumbani kwa baba yake. 3Yonathani akafanya agano na Daudi kwa sababu alimpenda kama nafsi yake mwenyewe. 4Yonathani akavua joho alilokuwa amevaa na kumpa Daudi, pamoja na koti lake, silaha zake, hata pamoja na upanga wake, upinde wake na mshipi wake. 5Lolote Sauli alilomtuma Daudi kufanya, alitenda kwa hekima, hata Sauli akampa cheo cha juu katika jeshi. Jambo hili likawapendeza watu wote, hata maafisa wa Sauli pia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.