Native Bible

1 Samuel 17:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Israeli na Wafilisti walikuwa wakipanga safu zao wakitazamana.

1 Samuel 17:21 in English

1 Samuel 17:21 · Berean Standard Bible

And Israel and the Philistines arrayed in formation against each other.

Context

19Wao wako pamoja na Sauli na watu wote wa Israeli huko kwenye Bonde la Ela, wakipigana na Wafilisti.” 20Asubuhi na mapema Daudi akaondoka, akaliacha kundi la kondoo pamoja na mchungaji, akapakia vitu vile na kuondoka, kama vile Yese alivyokuwa amemwagiza. Akafika kambini wakati jeshi lilikuwa likitoka kwenda kwenye sehemu yake ya kupigania, huku wakipiga kelele za vita. 21Israeli na Wafilisti walikuwa wakipanga safu zao wakitazamana. 22Daudi akaacha vile vitu vyake kwa mtunza vifaa, akakimbilia katika safu za vita na kuwasalimu ndugu zake. 23Alipokuwa akisema nao, Goliathi, yule Mfilisti shujaa kutoka Gathi, akajitokeza mbele ya safu zake na kupiga ile kelele yake ya kawaida ya matukano, naye Daudi akayasikia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.