1 Samweli 17:19
1 Samuel 17:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wao wako pamoja na Sauli na watu wote wa Israeli huko kwenye Bonde la Ela, wakipigana na Wafilisti.”
1 Samuel 17:19 in English
1 Samuel 17:19 · Berean Standard Bible
They are with Saul and all the men of Israel in the Valley of Elah, fighting against the Philistines.”
Context
17Wakati huo Yese akamwambia mwanawe Daudi, “Chukua hii efa* ya bisi na hii mikate kumi kwa ajili ya ndugu zako uwapelekee upesi kambini mwao. 18Chukua pamoja na hizi jibini kumi kwa jemadari wa kikosi chao. Ujue hali ya ndugu zako na uniletee taarifa za uhakika kutoka kwao. 19Wao wako pamoja na Sauli na watu wote wa Israeli huko kwenye Bonde la Ela, wakipigana na Wafilisti.” 20Asubuhi na mapema Daudi akaondoka, akaliacha kundi la kondoo pamoja na mchungaji, akapakia vitu vile na kuondoka, kama vile Yese alivyokuwa amemwagiza. Akafika kambini wakati jeshi lilikuwa likitoka kwenda kwenye sehemu yake ya kupigania, huku wakipiga kelele za vita. 21Israeli na Wafilisti walikuwa wakipanga safu zao wakitazamana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.