1 Samweli 17:17
1 Samuel 17:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati huo Yese akamwambia mwanawe Daudi, “Chukua hii efa* ya bisi na hii mikate kumi kwa ajili ya ndugu zako uwapelekee upesi kambini mwao.
1 Samuel 17:17 in English
1 Samuel 17:17 · Berean Standard Bible
One day Jesse said to his son David, “Take this ephah of roasted grain * and these ten loaves of bread for your brothers and hurry to their camp.
Context
15lakini Daudi alikuwa akienda kwa Sauli na kurudi ili kuchunga kondoo wa baba yake huko Bethlehemu. 16Kwa siku arobaini huyo Mfilisti alikuwa akija mbele kila siku asubuhi na jioni na kujionyesha. 17Wakati huo Yese akamwambia mwanawe Daudi, “Chukua hii efa* ya bisi na hii mikate kumi kwa ajili ya ndugu zako uwapelekee upesi kambini mwao. 18Chukua pamoja na hizi jibini kumi kwa jemadari wa kikosi chao. Ujue hali ya ndugu zako na uniletee taarifa za uhakika kutoka kwao. 19Wao wako pamoja na Sauli na watu wote wa Israeli huko kwenye Bonde la Ela, wakipigana na Wafilisti.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.