Native Bible

1 Samuel 17:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

lakini Daudi alikuwa akienda kwa Sauli na kurudi ili kuchunga kondoo wa baba yake huko Bethlehemu.

1 Samuel 17:15 in English

1 Samuel 17:15 · Berean Standard Bible

but David went back and forth from Saul to tend his father’s sheep in Bethlehem.

Context

13Wana wakubwa watatu wa Yese walikuwa wamefuatana na Sauli vitani: Mzaliwa wa kwanza alikuwa Eliabu, wa pili Abinadabu, na wa tatu Shama. 14Daudi ndiye alikuwa mdogo wa wote. Hao wakubwa watatu wakamfuata Sauli, 15lakini Daudi alikuwa akienda kwa Sauli na kurudi ili kuchunga kondoo wa baba yake huko Bethlehemu. 16Kwa siku arobaini huyo Mfilisti alikuwa akija mbele kila siku asubuhi na jioni na kujionyesha. 17Wakati huo Yese akamwambia mwanawe Daudi, “Chukua hii efa* ya bisi na hii mikate kumi kwa ajili ya ndugu zako uwapelekee upesi kambini mwao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.