1 Samweli 1:26
1 Samuel 1:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
naye Hana akamwambia Eli, “Hakika kama uishivyo, bwana wangu, mimi ndiye yule mama ambaye alisimama hapa karibu nawe akiomba kwa Bwana.
1 Samuel 1:26 in English
1 Samuel 1:26 · Berean Standard Bible
“Please, my lord,” said Hannah, “as surely as you live, my lord, I am the woman who stood here beside you praying to the LORD.
Context
24Baada ya mtoto kuachishwa kunyonya, Hana akamchukua huyo mtoto, akiwa mdogo hivyo hivyo, pamoja na fahali wa miaka mitatu, efa ya unga* na kiriba cha divai, naye akamleta mtoto kwenye nyumba ya Bwana huko Shilo. 25Walipokwisha kumchinja yule fahali, wakamleta mtoto kwa Eli, 26naye Hana akamwambia Eli, “Hakika kama uishivyo, bwana wangu, mimi ndiye yule mama ambaye alisimama hapa karibu nawe akiomba kwa Bwana. 27Niliomba mtoto huyu, naye Bwana amenijalia kile nilichomwomba. 28Hivyo sasa ninamtoa kwa Bwana. Kwa maana maisha yake yote atakuwa ametolewa kwa Bwana.” Naye akamwabudu Bwana huko.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.