Native Bible

1 Samuel 1:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baada ya mtoto kuachishwa kunyonya, Hana akamchukua huyo mtoto, akiwa mdogo hivyo hivyo, pamoja na fahali wa miaka mitatu, efa ya unga* na kiriba cha divai, naye akamleta mtoto kwenye nyumba ya Bwana huko Shilo.

1 Samuel 1:24 in English

1 Samuel 1:24 · Berean Standard Bible

Once she had weaned him, Hannah took the boy with her, along with a three-year-old bull,* an ephah of flour,* and a skin of wine. Though the boy was still young, she brought him to the house of the LORD at Shiloh.

Context

22Hana hakwenda. Alimwambia mume wake, “Baada ya mtoto kuachishwa kunyonya, nitamchukua na kumpeleka mbele za Bwana, naye ataishi huko wakati wote.” 23Elikana mumewe akamwambia, “Fanya lile unaloona ni bora zaidi kwako. Ukae hapa mpaka utakapomwachisha kunyonya, Bwana na akujalie kutimiza nadhiri yako.” Hivyo huyo mwanamke akakaa nyumbani na kumnyonyesha mwanawe mpaka alipomwachisha kunyonya. 24Baada ya mtoto kuachishwa kunyonya, Hana akamchukua huyo mtoto, akiwa mdogo hivyo hivyo, pamoja na fahali wa miaka mitatu, efa ya unga* na kiriba cha divai, naye akamleta mtoto kwenye nyumba ya Bwana huko Shilo. 25Walipokwisha kumchinja yule fahali, wakamleta mtoto kwa Eli, 26naye Hana akamwambia Eli, “Hakika kama uishivyo, bwana wangu, mimi ndiye yule mama ambaye alisimama hapa karibu nawe akiomba kwa Bwana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.