1 Wafalme 7:4
1 Kings 7:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Madirisha yake yaliwekwa juu kwa safu tatu, yakielekeana.
1 Kings 7:4 in English
1 Kings 7:4 · Berean Standard Bible
There were three rows of high windows facing one another in three tiers.
Context
2Alijenga Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni, urefu wake ulikuwa dhiraa 100,* upana wake dhiraa hamsini na kimo chake dhiraa thelathini,* likiwa na safu nne za nguzo za mierezi zikishikilia boriti za mierezi zilizorembwa. 3Ilipauliwa kwa mierezi juu ya boriti zile zilizolala juu ya nguzo arobaini na tano, kumi na tano kwa kila safu. 4Madirisha yake yaliwekwa juu kwa safu tatu, yakielekeana. 5Milango yote ilikuwa na miimo ya mstatili, ilikuwa upande wa mbele katika safu tatu, ikielekeana. 6Akajenga ukumbi wa nguzo, ambao urefu wake ulikuwa dhiraa hamsini* na upana wake dhiraa thelathini. Mbele ya jengo hilo kulikuwepo baraza. Mbele ya baraza kulikuwepo na nguzo na paa lililoningʼinia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.