1 Wafalme 7:6
1 Kings 7:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akajenga ukumbi wa nguzo, ambao urefu wake ulikuwa dhiraa hamsini* na upana wake dhiraa thelathini. Mbele ya jengo hilo kulikuwepo baraza. Mbele ya baraza kulikuwepo na nguzo na paa lililoningʼinia.
1 Kings 7:6 in English
1 Kings 7:6 · Berean Standard Bible
Solomon made his colonnade fifty cubits long and thirty cubits wide,* with a portico in front of it and a canopy with pillars in front of the portico.
Context
4Madirisha yake yaliwekwa juu kwa safu tatu, yakielekeana. 5Milango yote ilikuwa na miimo ya mstatili, ilikuwa upande wa mbele katika safu tatu, ikielekeana. 6Akajenga ukumbi wa nguzo, ambao urefu wake ulikuwa dhiraa hamsini* na upana wake dhiraa thelathini. Mbele ya jengo hilo kulikuwepo baraza. Mbele ya baraza kulikuwepo na nguzo na paa lililoningʼinia. 7Akajenga ukumbi wa kiti cha enzi, Ukumbi wa Hukumu, mahali ambapo angelitolea hukumu, akaufunika kwa mierezi kutoka sakafuni hadi darini. 8Kwenye jumba la kifalme ambamo angeliishi, aliiweka nyuma zaidi, ikiwa na mjengo wa aina moja na hiyo nyingine. Pia Solomoni akajenga jumba la kifalme linalofanana na huo ukumbi mkubwa kwa ajili ya binti Farao, aliyekuwa amemwoa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.