Native Bible

1 Kings 7:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Alijenga Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni, urefu wake ulikuwa dhiraa 100,* upana wake dhiraa hamsini na kimo chake dhiraa thelathini,* likiwa na safu nne za nguzo za mierezi zikishikilia boriti za mierezi zilizorembwa.

1 Kings 7:2 in English

1 Kings 7:2 · Berean Standard Bible

He built the House of the Forest of Lebanon a hundred cubits long, fifty cubits wide, and thirty cubits high,* with four rows of cedar pillars supporting the cedar beams.

Context

1Ilimchukua Solomoni miaka kumi na mitatu kukamilisha ujenzi wa Jumba lake la kifalme. 2Alijenga Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni, urefu wake ulikuwa dhiraa 100,* upana wake dhiraa hamsini na kimo chake dhiraa thelathini,* likiwa na safu nne za nguzo za mierezi zikishikilia boriti za mierezi zilizorembwa. 3Ilipauliwa kwa mierezi juu ya boriti zile zilizolala juu ya nguzo arobaini na tano, kumi na tano kwa kila safu. 4Madirisha yake yaliwekwa juu kwa safu tatu, yakielekeana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.