Native Bible

1 Kings 7:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ilimchukua Solomoni miaka kumi na mitatu kukamilisha ujenzi wa Jumba lake la kifalme.

1 Kings 7:1 in English

1 Kings 7:1 · Berean Standard Bible

Solomon, however, took thirteen years to complete the construction of his entire palace.

Context

1Ilimchukua Solomoni miaka kumi na mitatu kukamilisha ujenzi wa Jumba lake la kifalme. 2Alijenga Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni, urefu wake ulikuwa dhiraa 100,* upana wake dhiraa hamsini na kimo chake dhiraa thelathini,* likiwa na safu nne za nguzo za mierezi zikishikilia boriti za mierezi zilizorembwa. 3Ilipauliwa kwa mierezi juu ya boriti zile zilizolala juu ya nguzo arobaini na tano, kumi na tano kwa kila safu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.