Native Bible

1 Kings 4:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mahitaji ya Solomoni ya kila siku yalikuwa kori thelathini* za unga laini, kori sitini* za unga wa kawaida.

1 Kings 4:22 in English

1 Kings 4:22 · Berean Standard Bible

Solomon’s provisions for a single day were thirty cors of fine flour,* sixty cors of meal,*

Context

20Watu wa Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani; walikula, wakanywa na kufurahi. 21Mfalme Solomoni akatawala katika falme zote kuanzia Mto Frati hadi nchi ya Wafilisti, hadi kwenye mpaka wa Misri. Nchi hizi zilileta ushuru na zilikuwa chini ya Solomoni, siku zote za maisha yake. 22Mahitaji ya Solomoni ya kila siku yalikuwa kori thelathini* za unga laini, kori sitini* za unga wa kawaida. 23Ngʼombe kumi wa zizini, ngʼombe ishirini wa malisho, kondoo na mbuzi mia moja, pamoja na ayala, paa, kulungu na kuku wazuri sana. 24Kwa kuwa Solomoni alitawala falme zote magharibi ya mto, kuanzia Tifsa hadi Gaza, naye akawa na amani pande zote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.