1 Wafalme 22:47
1 Kings 22:47 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tangu hapo hapakuwepo na mfalme katika Edomu, naibu ndiye alitawala.
1 Kings 22:47 in English
1 Kings 22:47 · Berean Standard Bible
And there was no king in Edom; a deputy served as king.
Context
45Kwa habari ya matukio mengine ya utawala wa Yehoshafati, mafanikio aliyokuwa nayo na uhodari wake katika vita, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? 46Aliondolea mbali katika nchi mahanithi wa mahali pa kuabudia miungu waliobaki huko hata baada ya utawala wa baba yake Asa. 47Tangu hapo hapakuwepo na mfalme katika Edomu, naibu ndiye alitawala. 48Wakati huu Yehoshafati akaunda merikebu nyingi za biashara* ili kwenda Ofiri kuchukua dhahabu, lakini kamwe hazikusafiri, kwa maana zilivunjika huko Esion-Geberi. 49Wakati ule, Ahazia mwana wa Ahabu akamwambia Yehoshafati, “Waache watu wangu wasafiri baharini pamoja na watu wako,” lakini Yehoshafati akakataa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.