1 Wafalme 22:48
1 Kings 22:48 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati huu Yehoshafati akaunda merikebu nyingi za biashara* ili kwenda Ofiri kuchukua dhahabu, lakini kamwe hazikusafiri, kwa maana zilivunjika huko Esion-Geberi.
1 Kings 22:48 in English
1 Kings 22:48 · Berean Standard Bible
Jehoshaphat built ships of Tarshish * to go to Ophir for gold, but they never set sail, because they were wrecked at Ezion-geber.
Context
46Aliondolea mbali katika nchi mahanithi wa mahali pa kuabudia miungu waliobaki huko hata baada ya utawala wa baba yake Asa. 47Tangu hapo hapakuwepo na mfalme katika Edomu, naibu ndiye alitawala. 48Wakati huu Yehoshafati akaunda merikebu nyingi za biashara* ili kwenda Ofiri kuchukua dhahabu, lakini kamwe hazikusafiri, kwa maana zilivunjika huko Esion-Geberi. 49Wakati ule, Ahazia mwana wa Ahabu akamwambia Yehoshafati, “Waache watu wangu wasafiri baharini pamoja na watu wako,” lakini Yehoshafati akakataa. 50Kisha Yehoshafati akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi baba yake. Mwanawe Yehoramu akawa mfalme baada yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.