1 Wafalme 22:46
1 Kings 22:46 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Aliondolea mbali katika nchi mahanithi wa mahali pa kuabudia miungu waliobaki huko hata baada ya utawala wa baba yake Asa.
1 Kings 22:46 in English
1 Kings 22:46 · Berean Standard Bible
He banished from the land the male shrine prostitutes who remained from the days of his father Asa.
Context
44Yehoshafati pia alikuwa na amani na mfalme wa Israeli. 45Kwa habari ya matukio mengine ya utawala wa Yehoshafati, mafanikio aliyokuwa nayo na uhodari wake katika vita, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? 46Aliondolea mbali katika nchi mahanithi wa mahali pa kuabudia miungu waliobaki huko hata baada ya utawala wa baba yake Asa. 47Tangu hapo hapakuwepo na mfalme katika Edomu, naibu ndiye alitawala. 48Wakati huu Yehoshafati akaunda merikebu nyingi za biashara* ili kwenda Ofiri kuchukua dhahabu, lakini kamwe hazikusafiri, kwa maana zilivunjika huko Esion-Geberi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.