Native Bible

1 Corinthians 12:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule.

1 Corinthians 12:4 in English

1 Corinthians 12:4 · Berean Standard Bible

There are different gifts, but the same Spirit.

Context

2Mnajua kwamba mlipokuwa watu wasiomjua Mungu, kwa njia moja au ingine mlishawishika na kupotoshwa mkielekezwa kwa sanamu zisizonena. 3Kwa hiyo nawaambieni ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa na Roho wa Mungu anayeweza kusema, “Yesu na alaaniwe.” Pia hakuna mtu awezaye kusema, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu. 4Kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule. 5Kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni yule yule. 6Kisha kuna tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule atendaye kazi zote kwa watu wote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.