Native Bible

1 Corinthians 12:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa hiyo nawaambieni ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa na Roho wa Mungu anayeweza kusema, “Yesu na alaaniwe.” Pia hakuna mtu awezaye kusema, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu.

1 Corinthians 12:3 in English

1 Corinthians 12:3 · Berean Standard Bible

Therefore I inform you that no one who is speaking by the Spirit of God says, “Jesus be cursed,” and no one can say, “Jesus is Lord,” except by the Holy Spirit.

Context

1Basi ndugu zangu, kuhusu karama za rohoni, sitaki mkose kufahamu. 2Mnajua kwamba mlipokuwa watu wasiomjua Mungu, kwa njia moja au ingine mlishawishika na kupotoshwa mkielekezwa kwa sanamu zisizonena. 3Kwa hiyo nawaambieni ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa na Roho wa Mungu anayeweza kusema, “Yesu na alaaniwe.” Pia hakuna mtu awezaye kusema, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu. 4Kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule. 5Kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni yule yule.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.