Native Bible

1 Corinthians 12:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mnajua kwamba mlipokuwa watu wasiomjua Mungu, kwa njia moja au ingine mlishawishika na kupotoshwa mkielekezwa kwa sanamu zisizonena.

1 Corinthians 12:2 in English

1 Corinthians 12:2 · Berean Standard Bible

You know that when you were pagans, you were influenced and led astray to mute idols.

Context

1Basi ndugu zangu, kuhusu karama za rohoni, sitaki mkose kufahamu. 2Mnajua kwamba mlipokuwa watu wasiomjua Mungu, kwa njia moja au ingine mlishawishika na kupotoshwa mkielekezwa kwa sanamu zisizonena. 3Kwa hiyo nawaambieni ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa na Roho wa Mungu anayeweza kusema, “Yesu na alaaniwe.” Pia hakuna mtu awezaye kusema, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu. 4Kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.