Native Bible

1 Corinthians 10:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hivyo, yeye ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke.

1 Corinthians 10:12 in English

1 Corinthians 10:12 · Berean Standard Bible

So the one who thinks he is standing firm should be careful not to fall.

Context

10Msinungʼunike kama baadhi yao walivyofanya, wakaangamizwa na mharabu. 11Mambo haya yote yaliwapata wao ili yawe mifano kwa wengine, nayo yaliandikwa ili yatuonye sisi ambao mwisho wa nyakati umetufikia. 12Hivyo, yeye ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke. 13Hakuna jaribu lolote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Naye Mungu ni mwaminifu; hataruhusu mjaribiwe kupita mnavyoweza. Lakini mnapojaribiwa atawapa njia ya kutokea ili mweze kustahimili. 14Kwa hiyo wapenzi wangu, zikimbieni ibada za sanamu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.