Native Bible

1 Chronicles 25:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Pamoja na ndugu zao wote walikuwa wamefundishwa na kuwa stadi wa uimbaji kwa Bwana. Idadi yao walikuwa 288.

1 Chronicles 25:7 in English

1 Chronicles 25:7 · Berean Standard Bible

Together with their relatives, who were all trained and skillful in the songs of the LORD, they numbered 288.

Context

5Wote hawa walikuwa wana wa Hemani mwonaji wa mfalme. Aliwapata wana hawa kutokana na ahadi ya Mungu ili kumwinua. Mungu alimpa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu. 6Hawa wanaume wote walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao kwa ajili ya uimbaji katika Hekalu la Bwana wakitumia matoazi, zeze na vinubi, kwa ajili ya huduma katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya usimamizi wa mfalme. 7Pamoja na ndugu zao wote walikuwa wamefundishwa na kuwa stadi wa uimbaji kwa Bwana. Idadi yao walikuwa 288. 8Vijana kwa wazee, walimu kwa wanafunzi, wote walipanga kazi zao kwa kupiga kura. 9Kura ya kwanza, ambayo ilikuwa kwa ajili ya Asafu, ilimwangukia Yosefu, //wanawe na jamaa zake, 12 Ya pili ikamwangukia Gedalia, //yeye na wanawe pamoja na jamaa zake, 12

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.