1 Nyakati 25:8
1 Chronicles 25:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Vijana kwa wazee, walimu kwa wanafunzi, wote walipanga kazi zao kwa kupiga kura.
1 Chronicles 25:8 in English
1 Chronicles 25:8 · Berean Standard Bible
They cast lots for their duties, young and old alike, teacher as well as pupil.
Context
6Hawa wanaume wote walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao kwa ajili ya uimbaji katika Hekalu la Bwana wakitumia matoazi, zeze na vinubi, kwa ajili ya huduma katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya usimamizi wa mfalme. 7Pamoja na ndugu zao wote walikuwa wamefundishwa na kuwa stadi wa uimbaji kwa Bwana. Idadi yao walikuwa 288. 8Vijana kwa wazee, walimu kwa wanafunzi, wote walipanga kazi zao kwa kupiga kura. 9Kura ya kwanza, ambayo ilikuwa kwa ajili ya Asafu, ilimwangukia Yosefu, //wanawe na jamaa zake, 12
Ya pili ikamwangukia Gedalia, //yeye na wanawe pamoja na jamaa zake, 12 10Ya tatu ikamwangukia Zakuri, //wanawe na jamaa zake, 12
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.