Native Bible

1 Chronicles 2:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

(Lakini Geshuri na Aramu wakateka miji ya Hawoth-Yairi, pamoja na Kenathi na viunga vyake; jumla ilikuwa miji sitini.) Wote hawa walikuwa wazao wa Makiri babaye Gileadi.

1 Chronicles 2:23 in English

1 Chronicles 2:23 · Berean Standard Bible

But Geshur and Aram captured Havvoth-jair,* along with Kenath and its sixty surrounding villages. All these were descendants of Machir the father of Gilead.

Context

21Hatimaye, Hesroni akakutana kimwili na binti wa Makiri babaye Gileadi (ambaye alimwoa alipokuwa na umri wa miaka sitini), naye akamzaa Segubu. 22Segubu akamzaa Yairi, ambaye alitawala miji ishirini na mitatu katika Gileadi. 23(Lakini Geshuri na Aramu wakateka miji ya Hawoth-Yairi, pamoja na Kenathi na viunga vyake; jumla ilikuwa miji sitini.) Wote hawa walikuwa wazao wa Makiri babaye Gileadi. 24Baada ya Hesroni kufa huko Efrathi, Abiya mjane wa Hesroni akamzalia Ashuru, aliye baba wa Tekoa. 25Wana wa Yerameeli mzaliwa wa kwanza wa Hesroni walikuwa: Ramu mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.