Native Bible

1 Chronicles 18:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akaweka kambi za askari walinzi huko Edomu, nao Waedomu wote wakawa watumishi wa Daudi. Bwana akampa Daudi ushindi kila alipokwenda.

1 Chronicles 18:13 in English

1 Chronicles 18:13 · Berean Standard Bible

He placed garrisons in Edom, and all the Edomites were subject to David. So the LORD made David victorious wherever he went.

Context

11Mfalme Daudi akaviweka vifaa hivi wakfu kwa Bwana kama vile alivyokuwa amefanya kwa fedha na dhahabu aliyokuwa ameitwaa katika mataifa yote haya: Edomu na Moabu, Waamoni, Wafilisti na Waamaleki. 12Abishai mwana wa Seruya akawaua Waedomu 18,000 katika Bonde la Chumvi. 13Akaweka kambi za askari walinzi huko Edomu, nao Waedomu wote wakawa watumishi wa Daudi. Bwana akampa Daudi ushindi kila alipokwenda. 14Daudi akatawala Israeli yote, akitenda lililo haki na sawa kwa watu wake wote. 15Yoabu mwana wa Seruya alikuwa jemadari wa jeshi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mweka kumbukumbu;

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.