1 Nyakati 18:12
1 Chronicles 18:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Abishai mwana wa Seruya akawaua Waedomu 18,000 katika Bonde la Chumvi.
1 Chronicles 18:12 in English
1 Chronicles 18:12 · Berean Standard Bible
Moreover, Abishai son of Zeruiah struck down eighteen thousand Edomites in the Valley of Salt.
Context
10akamtuma mwanawe, Hadoramu kwa Mfalme Daudi ili kumsalimu na kumpongeza kwa ushindi wake katika vita dhidi ya Mfalme Hadadezeri, kwa kuwa alikuwa amepigana vita mara nyingi na Tou. Hadoramu akamletea Daudi vifaa mbalimbali vya dhahabu, fedha na shaba. 11Mfalme Daudi akaviweka vifaa hivi wakfu kwa Bwana kama vile alivyokuwa amefanya kwa fedha na dhahabu aliyokuwa ameitwaa katika mataifa yote haya: Edomu na Moabu, Waamoni, Wafilisti na Waamaleki. 12Abishai mwana wa Seruya akawaua Waedomu 18,000 katika Bonde la Chumvi. 13Akaweka kambi za askari walinzi huko Edomu, nao Waedomu wote wakawa watumishi wa Daudi. Bwana akampa Daudi ushindi kila alipokwenda. 14Daudi akatawala Israeli yote, akitenda lililo haki na sawa kwa watu wake wote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.