Native Bible

1 Chronicles 15:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Daudi akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu ili kulipandisha Sanduku la Bwana na kulileta hadi kwenye sehemu aliyokuwa ametengeneza kwa ajili yake.

1 Chronicles 15:3 in English

1 Chronicles 15:3 · Berean Standard Bible

And David assembled all Israel in Jerusalem to bring up the ark of the LORD to the place he had prepared for it.

Context

1Baada ya Daudi kujijengea nyumba zake katika Mji wa Daudi, akatengeneza sehemu kwa ajili ya Sanduku la Mungu, kisha akasimamisha hema kwa ajili yake. 2Kisha Daudi akasema, “Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kulibeba Sanduku la Mungu isipokuwa Walawi peke yao, kwa sababu Bwana aliwachagua kulibeba Sanduku la Bwana na kuhudumu mbele zake milele.” 3Daudi akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu ili kulipandisha Sanduku la Bwana na kulileta hadi kwenye sehemu aliyokuwa ametengeneza kwa ajili yake. 4Kisha Daudi akawakusanya pamoja wazao wa Aroni na Walawi: 5Kutoka wazao wa Kohathi, Urieli kiongozi na ndugu zake 120,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.