1 Nyakati 14:12
1 Chronicles 14:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wafilisti walikuwa wameacha miungu yao huko, Daudi akaamuru iteketezwe kwa moto.
1 Chronicles 14:12 in English
1 Chronicles 14:12 · Berean Standard Bible
There the Philistines abandoned their gods, and David ordered that they be burned in the fire.
Context
10Hivyo Daudi akamuuliza Mungu: “Je, niende kuwashambulia hao Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?”
Bwana akamjibu, “Nenda, nitawatia mikononi mwako.” 11Hivyo Daudi pamoja na watu wake wakakwea mpaka Baal-Perasimu,* akawashinda huko. Akasema, “Kama maji yafurikavyo, Mungu amewafurikia adui zangu kwa kutumia mkono wangu.” Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Baal-Perasimu. 12Wafilisti walikuwa wameacha miungu yao huko, Daudi akaamuru iteketezwe kwa moto. 13Kwa mara nyingine Wafilisti wakavamia lile bonde; 14hivyo Daudi akamuuliza Mungu tena, naye Mungu akamjibu, “Usiwapandie moja kwa moja, bali wazungukie na uwashambulie kutoka mbele ya hiyo miti ya miforosadi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.