1 Nyakati 14:13
1 Chronicles 14:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa mara nyingine Wafilisti wakavamia lile bonde;
1 Chronicles 14:13 in English
1 Chronicles 14:13 · Berean Standard Bible
Once again the Philistines raided the valley.
Context
11Hivyo Daudi pamoja na watu wake wakakwea mpaka Baal-Perasimu,* akawashinda huko. Akasema, “Kama maji yafurikavyo, Mungu amewafurikia adui zangu kwa kutumia mkono wangu.” Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Baal-Perasimu. 12Wafilisti walikuwa wameacha miungu yao huko, Daudi akaamuru iteketezwe kwa moto. 13Kwa mara nyingine Wafilisti wakavamia lile bonde; 14hivyo Daudi akamuuliza Mungu tena, naye Mungu akamjibu, “Usiwapandie moja kwa moja, bali wazungukie na uwashambulie kutoka mbele ya hiyo miti ya miforosadi. 15Mara usikiapo sauti ya kwenda juu ya hiyo miti ya miforosadi, hapo ndipo utoke upigane vita, kwa sababu hiyo itaonyesha kwamba Mungu amekutangulia ili kupiga jeshi la Wafilisti.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.