Sefania 2:13
Zephaniah 2:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mungu atanyoosha mkono wake dhidi ya kaskazini na kuangamiza Waashuru, akiiacha Ninawi ukiwa na pakame kama jangwa.
Zephaniah 2:13 in English
Zephaniah 2:13 · Berean Standard Bible
And He will stretch out His hand against the north and destroy Assyria; He will make Nineveh a desolation, as dry as a desert.
Context
11Bwana atakuwa wa kuhofisha kwao
atakapoangamiza miungu yote ya nchi.
Mataifa katika kila pwani yatamwabudu,
kila moja katika nchi yake. 12“Ninyi pia, ee Wakushi,
mtauawa kwa upanga wangu.” 13Mungu atanyoosha mkono wake dhidi ya kaskazini
na kuangamiza Waashuru,
akiiacha Ninawi ukiwa
na pakame kama jangwa. 14Makundi ya kondoo na ngʼombe yatajilaza pale,
viumbe vya kila aina.
Bundi wa jangwani na bundi waliao kwa sauti nyembamba
wataishi juu ya nguzo zake.
Mwangwi wa kuita kwao utapita madirishani,
kifusi kitakuwa milangoni,
boriti za mierezi zitaachwa wazi. 15Huu ndio mji uliotukuka na kuishi kwa furaha
wakijisikia salama.
Ulisema moyoni mwako,
“Mimi ndimi, na wala hapana mwingine ila mimi.”
Jinsi gani umekuwa gofu,
mahali pa kulala wanyama pori!
Wote wanaopita kando yake wanauzomea
na kutikisa mkono kwa dharau.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.