Native Bible

Zechariah 14:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Siku hiyo hakutakuwepo nuru, baridi wala theluji.

Zechariah 14:6 in English

Zechariah 14:6 · Berean Standard Bible

On that day there will be no light, no cold or frost.

Context

4Siku hiyo miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, mashariki mwa Yerusalemu, nao Mlima wa Mizeituni utagawanyika mara mbili kuanzia mashariki hadi magharibi, ukifanya bonde kubwa, nusu ya mlima ukisogea kuelekea kaskazini na nusu kuelekea kusini. 5Nanyi mtakimbia kupitia katika bonde hilo la mlima wangu kwa kuwa litaenea hadi Aseli. Mtakimbia kama mlivyokimbia tetemeko la ardhi katika siku za Uzia mfalme wa Yuda. Kisha Bwana Mungu wangu atakuja na watakatifu wote pamoja naye. 6Siku hiyo hakutakuwepo nuru, baridi wala theluji. 7Itakuwa siku ya kipekee, isiyo na mchana wala usiku, siku ijulikanayo na Bwana. Jioni inapofika nuru itakuwepo. 8Siku hiyo, maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu, nusu kwenda kwenye bahari ya mashariki,* na nusu kwenda kwenye bahari ya magharibi* wakati wa kiangazi na wakati wa masika.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.