Zekaria 14:8
Zechariah 14:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Siku hiyo, maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu, nusu kwenda kwenye bahari ya mashariki,* na nusu kwenda kwenye bahari ya magharibi* wakati wa kiangazi na wakati wa masika.
Zechariah 14:8 in English
Zechariah 14:8 · Berean Standard Bible
And on that day living water will flow out from Jerusalem, half of it toward the Eastern Sea * and the other half toward the Western Sea,* in summer and winter alike.
Context
6Siku hiyo hakutakuwepo nuru, baridi wala theluji. 7Itakuwa siku ya kipekee, isiyo na mchana wala usiku, siku ijulikanayo na Bwana. Jioni inapofika nuru itakuwepo. 8Siku hiyo, maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu, nusu kwenda kwenye bahari ya mashariki,* na nusu kwenda kwenye bahari ya magharibi* wakati wa kiangazi na wakati wa masika. 9Bwana atakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo atakuwepo Bwana mmoja na jina lake litakuwa jina pekee. 10Nchi yote kuanzia Geba, kaskazini mwa Yuda, hadi Rimoni, kusini mwa Yerusalemu, itakuwa kama Araba.* Lakini Yerusalemu utainuliwa juu na kubaki mahali pake, toka Lango la Benyamini hadi mahali pa Lango la Kwanza, mpaka kwenye Lango la Pembeni na kutoka Mnara wa Hananeli hadi kwenye mashinikizo ya divai ya mfalme.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.