Native Bible

Ruth 1:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Elimeleki mumewe Naomi akafa, hivyo Naomi akabaki na wanawe wawili.

Ruth 1:3 in English

Ruth 1:3 · Berean Standard Bible

Then Naomi’s husband Elimelech died, and she was left with her two sons,

Context

1Wakati Waamuzi walipotawala Israeli, kulikuwa na njaa katika nchi. Mtu mmoja kutoka nchi ya Bethlehemu ya Yuda, pamoja na mke wake na wanawe wawili, akaenda kuishi katika nchi ya Moabu. 2Mtu huyu aliitwa Elimeleki, mkewe aliitwa Naomi, na hao wanawe wawili waliitwa Maloni na Kilioni. Walikuwa Waefrathi kutoka Bethlehemu ya Yuda. Wakaenda katika nchi ya Moabu, wakaishi huko. 3Elimeleki mumewe Naomi akafa, hivyo Naomi akabaki na wanawe wawili. 4Nao wakaoa wanawake Wamoabu, jina la mmoja aliitwa Orpa, na wa pili aliitwa Ruthu. Baada ya kama miaka kumi, 5Maloni na Kilioni pia wakafa. Basi Naomi akabaki hana mume wala wanawe wawili.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.