Native Bible

Romans 3:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Tusemeje basi? Je, sisi ni bora kuwaliko wao? La hasha! Kwa maana tumekwisha kuhakikisha kwa vyovyote kwamba Wayahudi na watu wa Mataifa wote wako chini ya nguvu ya dhambi.

Romans 3:9 in English

Romans 3:9 · Berean Standard Bible

What then? Are we any better? Not at all. For we have already made the charge that Jews and Greeks alike are all under sin.

Context

7Mtu aweza kuuliza, “Kama uongo wangu unasaidia kuonyesha kweli ya Mungu na kuzidisha utukufu wake, kwa nini basi mimi nahukumiwa kuwa mwenye dhambi?” 8Nasi kwa nini tusiseme, kama wengine wanavyotusingizia kuwa tunasema, “Tutende maovu ili mema yapate kuja?” Wao wanastahili hukumu yao. 9Tusemeje basi? Je, sisi ni bora kuwaliko wao? La hasha! Kwa maana tumekwisha kuhakikisha kwa vyovyote kwamba Wayahudi na watu wa Mataifa wote wako chini ya nguvu ya dhambi. 10Kama ilivyoandikwa: “Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja. 11Hakuna hata mmoja mwenye ufahamu, hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.