Warumi 10:15
Romans 10:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nao watahubirije wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, “Tazama jinsi ilivyo mizuri miguu yao wale wanaohubiri habari njema!”
Romans 10:15 in English
Romans 10:15 · Berean Standard Bible
And how can they preach unless they are sent? As it is written: “How beautiful are the feet of those who bring good news!”*
Context
13Kwa maana, “Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokolewa.” 14Lakini watamwitaje yeye ambaye hawajamwamini? Nao watawezaje kumwamini yeye ambaye hawajamsikia? Tena watamsikiaje bila mtu kuwahubiria? 15Nao watahubirije wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, “Tazama jinsi ilivyo mizuri miguu yao wale wanaohubiri habari njema!” 16Lakini si wote waliotii Habari Njema. Kwa maana Isaya asema, “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?” 17Basi, imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.