Warumi 1:13
Romans 1:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba mara nyingi nimekusudia kuja kwenu (ingawa mpaka sasa nimezuiliwa), ili nipate kuvuna mavuno miongoni mwenu kama nilivyovuna miongoni mwa wengine ambao ni watu wa Mataifa wasiomjua Mungu.
Romans 1:13 in English
Romans 1:13 · Berean Standard Bible
I do not want you to be unaware, brothers, how often I planned to come to you (but have been prevented from visiting * until now), in order that I might have a harvest among you, just as I have had among the other Gentiles.
Context
11Ninatamani sana kuwaona ili nipate kuweka juu yenu karama za rohoni ili mwe imara, 12au zaidi, ninyi pamoja nami tuweze kutiana moyo katika imani sisi kwa sisi. 13Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba mara nyingi nimekusudia kuja kwenu (ingawa mpaka sasa nimezuiliwa), ili nipate kuvuna mavuno miongoni mwenu kama nilivyovuna miongoni mwa wengine ambao ni watu wa Mataifa wasiomjua Mungu. 14Mimi ni mdeni kwa Wayunani na kwa wasio Wayunani, kwa wenye hekima na kwa wasio na hekima. 15Ndiyo sababu ninatamani sana kuihubiri Injili kwenu pia ninyi mlioko Rumi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.