Ufunuo 9:8
Revelation 9:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Walikuwa na nywele kama za wanawake, na meno yao yalikuwa kama ya simba.
Revelation 9:8 in English
Revelation 9:8 · Berean Standard Bible
They had hair like that of women, and teeth like those of lions.
Context
6Katika siku hizo watu watatafuta kifo lakini hawatakiona, watatamani kufa, lakini kifo kitawakimbia. 7Wale nzige walikuwa na umbo kama la farasi waliotayarishwa kwa ajili ya vita. Kwenye vichwa vyao kulikuwa na kitu kama taji za dhahabu na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu. 8Walikuwa na nywele kama za wanawake, na meno yao yalikuwa kama ya simba. 9Walikuwa na dirii kama za chuma, na sauti za mabawa yao zilikuwa kama ngurumo za farasi wengi na magari mengi yakikimbilia vitani. 10Walikuwa na mikia yenye miiba ya kuumia kama nge. Nguvu yao ya kutesa watu kwa huo muda wa miezi mitano ilikuwa katika hiyo mikia yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.